Mbappe aweka rekodi ya ufungaji magoli PSG

Kylian Mbappe amekuwa mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli mengi katika timu ya Paris St-Germain kwenye Ligue 1 wakati wakiifunga 3-1 Lens iliyosalia na wachezaji 10, na kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.

Mbappe, ambaye amefikisha idadi ya magoli 139 katika mechi 169 za ligi kuu ya Ufaransa alizocheza amepita idadi ya magoli yaliyofungwa na Edinson Cavani.

Katika mchezo huo muhimu wa ligi hiyo dhidi timu mbili za juu katika msimamo wa ligi, kiungo wa Lens Salis Abdul Samed alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 19 ya mchezo.

Lionel Messi na Vitinha nao pia waliifungia magoli PSG kabla ya Przemyslaw Frankowski kuifungia Lens goli pekee kwa mkwaju wa penati.

Chanzo: BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni