Raila kuanzisha upya maandamano dhidi ya serikali

 

Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga, leo anaanza mfululizo wa mikutano ya kuhamasisha maandamano mengine, baada mazungumzo yake na Rais William Ruto kuwa na uwezekano wa kutofanyika.

Odinga ataongoza mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kamukunji Jijini Nairobi, ikiwa ni siku moja tu kupita tangu kutangaza kurejesha tena maandamano, baada ya kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Washirika wake wameliambia gazeti la Sunday Nation jana kwamba wameandaa mfululizi wa mikutano kuhamasisha maandamano, siku moja tu baada wafuasi wa rais Ruto kutishia kujitoa kwenye mazungumzo.

Odinga amewashirikisha wanaharakati wa haki za binadamu, taasisi za kidini, vyama vya wanafunzi, vyama vya wafanyakazi, vyama vya wakulima, wafanyabiashara wadogo na tasisi za kijamii katika mipango yake ya maandamano.

Chama cha upinzani cha Azimio la Umoja, kinatarajia kuungwa mkono kutokana na kupanda kwa gharama za maisha na mgogoro wa kifedha ambapo taifa hilo limeshuhudia serikali ikishindwa kutoa mafungu ya fedha ya kuendesha Kaunti na kuchelewesha mishahara ya watumishi wa umma.

Chapisha Maoni

0 Maoni