Mbunge wa Tarime Vijijini,
Mwita Waitara, ameweka msimamo mkali Bungeni jijini Dodoma akiwataka
viongozi wanaotoa matamko yanayozua taharuki na mifarakano kuondolewa
kwenye nafasi zao mara moja, akisisitiza kuwa hawafai kuendelea
kushika nyadhifa za uongozi.
Akichangia Hotuba ya Bajeti Kuu
ya Serikali na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2026/27,
Waitara amesema haiwezekani baadhi ya watu “kutoboa mtumbwi” huku
wengine wakikaa kimya bila kuchukua hatua za kinidhamu.
Amesema
kauli na matendo ya viongozi yanapaswa kulinda umoja wa taifa badala
ya kuchochea mgawanyiko au hofu miongoni mwa wananchi.
Aidha,
amewataka Wabunge na viongozi wa ngazi mbalimbali kuheshimu wananchi
na kuchunga maneno yao ili kuepuka kuibua taharuki isiyo ya lazima na
kudumisha mshikamano wa kitaifa.

0 Maoni