Umoja wa Waendesha Magari
ya Biashara (Kirikuu) wa Manzese, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es
Salaam, umewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani ili
kuhakikisha shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kufanyika kwa
utulivu na maendeleo.
Wakizungumza jijini Dar es Salaam,
madereva hao wamesema amani ni msingi muhimu wa maendeleo ya taifa,
hivyo kila mwananchi ana wajibu wa kuilinda, kuiendeleza na kuienzi
kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha, wamewaomba
vijana kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga utulivu wa nchi,
wakisisitiza kuwa amani ndiyo nguzo kuu ya ukuaji wa uchumi, ustawi
wa jamii na kuboresha maisha ya wananchi.
Madereva hao
wameeleza kuwa mazingira ya amani na utulivu huwezesha wananchi
kufanya shughuli zao za uzalishaji kwa uhuru na kuchangia maendeleo
ya taifa.

0 Maoni