Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka vijana kuendelea
kulinda amani na utulivu wa nchi kwa wivu mkubwa akisisitiza kuwa
amani ndiyo msingi wa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa
ujumla.
Faris amesema hayo alipokuwa akizungumza na vijana wa
Bukoba Mjini katika mwendelezo wa Operesheni ya Vijana Daka Fursa na
Samia (VIDAFUSA) inayotekelezwa na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM
Mkoa wa Kagera.
Amesema bila amani na utulivu, juhudi za
maendeleo, uwekezaji na fursa za kiuchumi kwa vijana haziwezi
kufanikiwa, hivyo kila kijana ana jukumu la kuwa balozi wa mshikamano
na umoja katika jamii.
Aidha, amewahimiza vijana kutumia fursa
mbalimbali zinazotolewa na Serikali kujikwamua kiuchumi na kuchangia
maendeleo ya Taifa badala ya kujihusisha na vitendo vinavyoweza
kuhatarisha amani ya nchi.

0 Maoni