Washiriki zaidi ya 300 wameshiriki
mbio fupi za kilomita 5 katika bonde la Olduvai Ngorongoro kwa lengo
la kutangaza vivutio vya asili vya Olduvai na Laetoli ambapo historia
ya Binadamu wa Kale ilianzia.
Akizungumza kwa Niaba ya
Kamishna wa Uhifadhi kwenye tukio hilo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Uhifadhi anayesimamia Huduma za Utalii na Masoko Mariam Kobelo
ameeleza kuwa Ngorongoro kwa kushirikiana na Cape to Cairo Marathon
imefanya mbio hizo ili kuonesha utajiri wa utalii wa asili, historia,
urithi wa utamaduni na mambo kale uliopo Olduvai na Laetoli kama
Nyumbani kwa asili ya Binadamu.
Ameongeza kuwa Ngorongoro ni Nyumbani kwa Nyumbu wanaohama kwa kuwa pumzi ya kwanza ya ndama kupigwa mhuri kabla ya kuhamia maeneo mengine safari yao huanzia Ndutu Ngorongoro.
"Ngorongoro
ni Nyumbani kwa asili ya binadamu kisayansi, Ni nyumbani kwa Nyumbu
wanaohama kila mwaka, ni nyumbani kwa Spinshi ya Ndege zaidi ya 500,
ni nyumbani kwa Wanyama wakubwa watano, kiufupi eneo la Ngorongoro ni
Nyumbani kwa mkusanyiko wa Vitu vingi ndio maana tunawaambia wadau
wote ndani na nje ya Nchi kuwa Wonders Are Calling" ameongeza
Kamishna Kobelo.
Mkurugenzi wa Cape to Cairo Arusha
International Marathon, Timothy Mdinka ameeleza kuwa lengo la mbio
hizo ni kutangaza mazao mapya ya Utalii yaliyopo Tanzania na Bara la
Africa kwa Ujumla kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo Michezo kama
mbio ambayo imefanyika leo Olduvai pamoja na marathon ya Cape to
Cairo itakayofanyika tarehe 31 Mei, 2026.
Mbio hizo
zimejumuisha wadau mbalimbali wakiwepo Ngorongoro, Cape to Cairo
international Marathon, Karatu Runners, Amani Collection, CRDB,
UNDP, NHIF, Diplomatic and Tourism Police Arusha.



0 Maoni