Kumekuwa na mwitikio mkubwa wa
watalii wa ndani kutembelea hifadhi ya Ngorongoro hii ikimaanisha
wanarudi nyumbani eneo ambalo ndilo pekee lenye ushahidi wa kisayansi
usiotiliwa shaka kuwa ndio chanzo cha binadamu wa kale.
Safari
hii ni zamu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) chini
ya Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Kijitonyama jijini
Dar es Salaam Rev, Dr. Elliona Kimaro aliyeongoza kundi la wanaume
300 kutoka mikoa mbalimbali nchini kutembea Makumbusho ya Jiopaki ya
Ngorongoro-Lengai (Urithi Geopark) na vituo vya hifadhi vilivyopo
Ngorongoro
Akiwa na Ujumbe huo Dkt. Kimaro amesema makundi
mbalimbali kuhamasika kufanya utalii wa Ndani wanavutiwa na vitu
mbalimbali ikiwemo kushuhudia uumbaji wa Mungu, kuona na kujifunza
Chanzo cha asili ya Mwanadamu katika bonde la Olduvai na Laetoli,
kuona Ikolojia ya hifadhi pamoja na utunzaji wa Mazingira kama vitabu
vitakatifu vinavyohimiza.
"Tumekuja Nyumbani Ngorongoro
kwenye asili ya Mwanadamu tukiwa na kundi la wanaume 300,
tumeshuhudia uumbaji wa Mungu, utunzaji wa Ikolojia, Mazingira,
Misitu Wanyama wa kila aina ya vyote vilivyoumbwa kwa mfano wa Mungu"
alisema Dkt. Kimaro.
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
inawarudisha nyumbani binadamu wote ili kushuhudia asili yao ambapo
binadamu alianza kutembea na kufanya shughuli zake kwa miguu miwili.


.jpeg)
0 Maoni