Baada
ya kuwasilishwa kwa ripoti ya matukio ya vurugu ya Oktoba 29, 2025,
wadau wa siasa na diplomasia wamesisitiza kuwa mustakabali wa taifa
unapaswa kujengwa juu ya maridhiano na kuaminiana ili kurejesha imani
ya wananchi na kudumisha utulivu wa nchi.
Akizungumza katika
mahojiano na vyombo vya habari vya kimataifa hivi karibuni, Mshauri
wa Rais wa Diplomasia, Lazaro Nyalandu, amesema kuwa jukumu la msingi
la Serikali ni kulinda usalama wa wananchi wake wakati
wote.
Ameeleza kuwa kauli za Samia Suluhu Hassan zinaonesha
dhamira ya kweli ya kutafuta suluhu ya kudumu, huku akisisitiza kuwa
msingi mkubwa wa kufanikisha hilo ni kujenga kuaminiana miongoni mwa
pande zote.
Aidha, amebainisha kuwa Tume iliyoongozwa na
Othman Chande imekamilisha kazi yake na kuwasilisha ripoti, ambayo
imeweka wazi baadhi ya ukweli kuhusu changamoto zilizokuwa
zikilikumba taifa pamoja na hatua zilizochukuliwa na Serikali.
Kwa
mujibu wa Nyalandu, ripoti hiyo imeonyesha ushahidi unaoeleza namna
baadhi ya waandamanaji walivyoshiriki katika vurugu hizo, wakiwa na
silaha mbalimbali ikiwemo bunduki na vilipuzi, huku wengine wakidaiwa
kupata mafunzo maalum katika kambi tofauti.
Ameongeza kuwa kwa
kuzingatia maelezo ya tume, matukio ya Oktoba 29, 2025 yalikuwa na
viashiria vya kupangwa, hali iliyosababisha Serikali kuchukua hatua
za haraka kulinda maisha ya wananchi, akibainisha kuwa ilikuwa siku
yenye majonzi na changamoto kubwa kwa kila Mtanzania.
#UmojaWetuNdiyoNguvuYetu
#turidhiane

0 Maoni