Wimbi kubwa la hasira na uzalendo limeendelea kutawala
katika mitandao ya kijamii, hususan Instagram, ambapo maelfu ya wananchi
wameibuka kupinga kile wanachokiita "ushetani na tamaa ya madaraka"
inayolenga kuivuruga Tanzania.
Hali hii inakuja baada ya kusambaa kwa video na kauli
zinazodaiwa kuchochea uvamizi wa kijeshi na machafuko nchini, jambo ambalo
Watanzania wameliandama kwa maneno makali.
Kwenye maoni yaliyofurika mtandaoni, wananchi wameonyesha
kuchoshwa na harakati za watu binafsi na makundi yanayotumia mwamvuli wa dini
na siasa kuvunja utulivu wa nchi.
Mmoja wa watumiaji wa Instagram ametoa ujumbe mzito
akisema, "Amani yetu ni nguzo yetu," huku wengine wakihoji dhamira ya
wale wanaoomba nchi ivamiwe, wakisema: "Sijui hawa watu wanataka nini,
ushetani unaowaingia hawajui madhara yake."
Mjadala huo haujawaacha salama viongozi wa dini na vyama
vya siasa vinavyotajwa kuhusika na harakati hizo. Wananchi wengi wameelekeza
lawama kwa Padri Kitima na baadhi ya washirika wa vyama vya upinzani, wakidai
kuwa wamejificha kwenye kivuli cha "kudai haki" ili kutimiza matamanio
yao ya madaraka.
"Wanadai haki kivuli cha maovu yao, wanataka madaraka
hawa tamaa inawasumbua," aliandika mdau mwingine.
Hisia za wananchi zimeonyesha kuwa Watanzania wa leo
wameerevuka na hawako tayari kutumika kama daraja la machafuko. Wengi wamesisitiza
kuwa yeyote anayeota kuona damu ikimwagika nchini anapaswa kukabiliwa kwa mkono
wa chuma wa sheria.
Kuna waliokwenda
mbali zaidi na kusema, "Waunde tu kundi la uasi wauawe kihalali,"
ikionyesha kiwango cha juu cha uchungu walionao wananchi dhidi ya wanaotaka
kuharibu amani iliyodumu kwa miongo mingi.
Licha ya presha na hamasa za hapa na pale, kauli mbiu
iliyotawala ni moja: Tanzania ni nchi ya amani na tuko nyuma ya Rais wetu.
Wananchi wametoa onyo kuwa michezo yoyote ya kitoto inayolenga kuyumbisha
uchumi na usalama wa nchi haitafanikiwa, kwani "Amani ni ngao ya nchi yetu
na tuilinde kwa gharama yoyote."

0 Maoni