Picha
zinazoonesha ushirikiano wa karibu kati
ya wachochezi wa vurugu za Oktoba 29 na
shirika kubwa la kimataifa la habari, CNN zimeendelea kuvuja huku watumiaji wa
mitandao wakielezea ushirikiano huo haramu ukiwa ni sehemu ya "mradi"
mpana unaolenga kuchafua taswira ya Tanzania na kuhamasisha vurugu ili kufikia
lengo la kuangusha Serikali iliyopo madarakani.
Miongoni mwa picha
hizo ni hii inayomuonesha Maria Sarungi akizungumza na mwandishi wa CNN,
Mwandishi Larry Madowo raia wa Kenya ambaye aliandika makala yenye uwongo
mkubwa ikiwamo kuwapo kwa kaburi la jumla pale kwa Kondo akidai ni picha za
setelaiti.
Hata hivyo,
wanamtandao wanahoji kuwa Chadema pamoja na wanaharakati wao hawajaenda
kuonesha makaburi hayo yanayotajwa na Satellite "fake" ya CNN.
Imeelezwa katika
mitandao kuwa Maria Sarungi ndiye aliyempatia malipo mwandishi huyo kwa kazi ya kuufanya uchafuzi ndani ya CNN
dhidi ya Tanzania.
Mwandishi huyo wa
CNN alijaribu kutumia ushawishi wake kuaminisha umma kwamba shirika hilo
lilikuwa na picha za satelaiti zinazothibitisha uwepo wa makaburi hayo.

0 Maoni