Wanawake wa
Tanzania, kupitia UWT Taifa na Mwenyekiti Mary Chatanda, wametangaza rasmi
makubaliano muhimu yenye vifungu vinavyolenga kuimarisha amani nchini. Wito wao
mkubwa ni kwa wanawake wote kudumisha upendo, heshima, mazungumzo na
kusameheana.
Msimamo wa
Wanawake: Wanawake wameahidi kuiheshimu, kuitunza, na kuimarisha amani ya
Tanzania. Wanasisitiza kuwa hakuna maendeleo yatakayopatikana bila amani, na
ndiyo maana wanapinga aina zote za rushwa na migogoro mikubwa na midogo
inayohatarisha utulivu.
Kukataa Vurugu na
Upotoshaji: Azimio hili linakataa vikali vitendo vya ukosefu wa amani,
udhalilishaji, unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji, ukatili, pamoja na matumizi
mabaya ya mitandao ya kijamii yanayosababisha chuki na mifarakano. Wameahidi
kupinga taarifa potofu, lugha za chuki na kazi zinazoleta mpasuko katika jamii.
Ushirikiano na
Malezi Bora: Wanawake wamejitolea kuimarisha ushirikiano katika familia na
jamii nzima ili kulinda mshikamano. Pia, wameahidi kuendeleza malezi mazuri na
mienendo mwema kwa watoto na vijana ili kukataa utamaduni wa kusikiliza sauti
za mitandaoni zinazochochea chuki.
Ujumbe kwa Vijana:
Mary Chatanda amewataka vijana waache kutumika kwa maslahi ya kisiasa. Ametoa
wito kuwa makini na kinachoendelea katika mitandao na kujiepusha nayo kwa
maslahi mapana ya taifa.

0 Maoni