Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Bwana Abdul-Razaq Badru amezipongeza timu za Mamlaka hiyo zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya serikali na Taasisi Binafsi (SHIMMUTA) yanayoendelea mkoani Morogoro kwa kuendelea kulinda na kutangaza taswira ya taasisi hiyo kupitia sekta ya Michezo.
Akitoa salamu
alipotembelea timu hiyo kwa niaba
Kamishna Badru, Kaimu Meneja wa Uhusiano kwa umma bwana Hamis Dambaya
amesema menejimenti ya Ngorongoro imeridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na
timu hizo katika mashindano hayo na kulitangaza shirika kupitia utalii wa
michezo (sport tourism).
Katika mashindano hayo Ngorongoro imefanikiwa kutwaa
Medali saba huku ikidhihirisha upekee wake kimataifa na kuendelea kuwa Premium
Safari Destination.



0 Maoni