Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mheshimiwa Mobhare
Matinyi, akisalimiana na Mfalme Carl XVI Gustaf wa Sweden, kwenye Kasri la
Mfalme jijini Stockholm, tarehe 9 Desemba, 2025. Kushoto ni Binti Mrithi wa
Ufalme, Victoria, katikati ni Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya
Sweden, Balozi Maria Christina Lundqvist, na kulia ni Mke wa Balozi, Yvonne
Matinyi. Katika mazungumzo yao mafupi, Mfalme Gustaf na Balozi Matinyi
walijadiliana kuhusu uimarishaji wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili,
hususani, katika nyanja za biashara, uwekezaji na utalii. (Picha kwa hisani ya
Kasri la Mfalme).

0 Maoni