Zaidi ya
watu 58 wamenufaika na programu ya usimamizi wa maji taka migodini,
inayotekelezwa kuanzia mwaka 2018 hadi 2025 chini ya usimamizi wa Taasisi ya
Jiolojia ya Sweden (SGU) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la
Sweden (SIDA).
Hayo yamesemwa
leo Oktoba 2, 2025 na Meneja wa Mradi wa Mafunzo ya Kimataifa kutoka SGU, Bi.
Jonnina Karlsson, wakati wa ziara yake katika Ofisi za Wizara ya Madini na
kushiriki kikao kilichoongozwa na Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga,
jijini Dodoma.
Katika
kikao hicho, Bi. Karlsson ameeleza kuwa hivi karibuni kutakuwa na fursa
nyingine kupitia mradi wa PanGeo+ ambao utatoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta
ya Madini, hususan katika masuala ya kiufundi na usimamizi endelevu wa
mazingira.
Aidha,
Bi. Karlsson ameonesha nia ya kufahamu mahitaji ya wataalamu wa Sekta ya Madini
nchini, ambapo imebainishwa kuwa miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na
mwongozo wa ufungaji wa migodi kwa wachimbaji wadogo; Upimaji wa maji taka
kabla ya kurejeshwa kwenye mazingira, hasa kwa wachimbaji wadogo na Matumizi ya
teknolojia za Remote Sensing na mifumo ya taarifa za jiolojia (GIS) katika
utafutaji wa madini pamoja na kujenga uwezo wa watalaam katika mchakato wa
kisayansi na kiuhandisi hususan katika kutathmin.
Mahitaji
mengine ni kujengewa uwezo katika kupanga na kuonyesha kiasi cha ubora wa
rasilimani kama vile madini yaani
Resource modelling kwa ajili ya kusaidia kufanya maamuzi sahihi katika
utekelezaji wa miradi ya madini.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Madini Dkt. Abdulrhaman Mwanga ameishukuru SIDA
kupitia SGU kwa kuwezesha mafunzo hayo ambayo yamelenga kuongeza uelewa kwa
wataalamu wa madini kuhusu usimamizi wa madini pamoja na miundombinu ya maji
taka migodini, hatua inayosaidia kulinda mazingira na kukuza uchimbaji endelevu.


0 Maoni