JWTZ yakemea uchochezi mitandaoni, yasisitiza kutohusishwa na siasa

 

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetoa taarifa kwa umma likikemea vitendo vya baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuweka maudhui yenye lengo la kuchochea kuliingiza Jeshi katika mambo ya siasa.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa JWTZ, Kanali Bernard Masala Mlunga, imesema jeshi lilibainisha kuwa baadhi ya hoja zinazochochea siasa hutolewa na watu walio katika mazingira ya kijeshi, wale wanaojinasibisha na Jeshi, au waliokuwa wameachishwa Jeshi kutokana na tabia na mwenendo mbaya, pamoja na kujihusisha na siasa na uanaharakati.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limeuarifu umma wa Watanzania kuwa litaendelea kutekeleza majukumu yake Kikatiba na kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chao, imemalizia taarifa hiyo.



Chapisha Maoni

0 Maoni