Mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi amefanya mkutano wake wa hadhara wa wa kampeni leo Oktoba 15, 2025 katika kata ya Puma wilaya ya Ikungi ndani ya Jimbo la Ikungi Magharibi mkoani Singida.
Akiwa
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi aliinadi Sera na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) ya 2025-2030 kwa Wananchi ikiwemo na kuwaomba kumpigia kura za ushindi wa kishindo Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.
Aidha, Dkt.
Nchimbi pia alitumia nafasi hiyo kuwanadi baadhi ya wagombea Ubunge wa mkoa huo
akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Ikungi Magharibi Ndugu Elibariki Immanuel
Kingu, mgombea Ubunge jimbo la Ikungi Mashariki Ndugu Thomas Mgonto KITIMA na
Madiwani.
Balozi
Nchimbi anafikia mkoa wa 23 sasa tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti
28,2025 jijini Dar es Salaam,akiendelea kusaka kura za ushindi wa kishindo za
mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Dkt. Samia
Suluhu Hassan,Wabunge na Madiwani.




0 Maoni