Kwa mujibu wa ripoti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
ya mwezi Septemba 2025 imeeleza kwamba rekodi ya madini ya dhahabu imepanda hadi kufikia dola za Marekani
bilioni 4.3 katika soko la dunia.
Ripoti ya BoT
imeeleza kwamba, uuzaji wa bidhaa za huduma nje ya nchi umeongezeka kwa
asilimia 14.8 kwa mwaka na kufikia jumla ya dola za Kimarekani 16,894.4 mwishoni mwa mwezi Agosti 2025.
BoT imefafanua kuwa , kwa upande wa uuzaji wa
dhahabu uliongezeka kwa asilimia 35.5 na kufikia dola milioni 4, 322.3 kutokana
na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia.
Ikielezea kuhusu mauzo ya bidhaa kutoka Sekta ya Kilimo ripoti imeeleza
kuwa, katika mwezi husika mauzo yaliongezeka hadi kufikia dola milioni 1,411.7
ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia 28.3 lililotokana na mauzo ya korosho,
tumbaku na kahawa.
Pamoja na dhahabu mauzo mengine ni bidhaa za viwandani, korosho
Tumbaku na nafaka.
0 Maoni