Mgombea
Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, na chama
chake wamefanikiwa kudhihirisha wazi kwamba wanatosha na wameiandaa Tanzania
kwa hatua kubwa inayofuata ya maendeleo, huku wakikabiliana na wapotoshaji
wachache kwa kutumia lugha moja tu: Matokeo Yanayopimika.
Tukielekea
Uchaguzi Mkuu, kuna jambo moja lisilopingika: Ukweli hauwezi kufichwa.
Wanaojaribu kufunika jitihada kubwa za maendeleo nchini wamejikuta wakiumia kwa
sababu jua la mafanikio linaangaza kila kona ya taifa.
Dkt.
Samia alikabidhiwa nchi wakati ikiwa kwenye majonzi, lakini badala ya
kutetereka, alisimama imara. Ameiweka Tanzania katika viwango vipya vya uongozi
vinavyopimika si kwa maneno matupu, bali kwa takwimu na matokeo yanayoonekana
kwa macho.
Mageuzi Makubwa katika Nishati na Elimu
Chini ya
uongozi wake, sekta ya Nishati imeshuhudia mabadiliko makubwa. Uzalishaji wa
umeme nchini umeongezeka kutoka megawati 1,602 mwaka 2020 hadi kufikia megawati
3,078 mwaka 2024. Ongezeko hili kubwa, ambalo linatokana kwa kiasi kikubwa na
mradi wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP), linatoa uhakika wa umeme wa
kutosha kwa viwanda na matumizi ya nyumbani.
Sambamba
na hilo, dhamira ya kupeleka umeme hadi vijijini imeimarika, ambapo vijiji
vyenye umeme vimeongezeka kutoka 8,587 mwaka 2020 hadi kufikia 12,318 mwaka
2024. Hii ni ishara ya wazi ya kuondoa giza na kupeleka maendeleo kwa wananchi
wa hali ya chini.
Katika
sekta ya Elimu, namba zinaonesha ari mpya. Idadi ya shule za msingi imeongezeka
kutoka 16,656 mwaka 2020 hadi 19,783 mwaka 2024, huku shule za sekondari
zikipanda kutoka 5,000 hadi 5,929. Hatua hii inahakikisha watoto wa Kitanzania
wanapata nafasi za kutosha za elimu bora kuanzia chini hadi juu.
Afya na Uchumi wa Mwananchi Zaimarishwa
Uboreshaji
wa sekta ya Afya pia umekuwa kipaumbele. Upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
umeimarika kutoka asilimia 75.6% mwaka 2020 hadi asilimia ya kuvutia ya 89.3%,
hatua inayoimarisha huduma za afya nchini kote.
Katika
kusaidia wananchi wengi, Serikali imewekeza katika sekta za uzalishaji.
Matumizi ya mbolea kwenye Kilimo yameongezeka kutoka tani 586,604 mwaka 2020 hadi
zaidi ya milioni 1.2 mwaka 2024. Aidha, eneo linalotumia umwagiliaji limepanda
kwa kasi kutoka hekta 561,383 hadi 983,466, hatua muhimu ya kuifanya kilimo
kisitegemee mvua.
Katika
sekta ya Uvuvi, wavuvi wamewezeshwa kwa ongezeko la boti za kisasa kutoka 280
mwaka 2020 hadi 507 mwaka 2024, na hivyo kuongeza tija na kipato chao.
Propaganda Zatafunwa na Ukweli
Haya yote
ni ushahidi wa dhahiri kwamba Mama Samia si kiongozi wa maneno, bali wa matokeo
ya kweli. Wanaojaribu kupotosha ukweli huu wanapaswa kuelewa kuwa Tanzania ipo
kwenye njia ya maendeleo isiyozuilika.
Kazi na
utekelezaji vinafanywa kwa vitendo, na jitihada zozote za kutumia propaganda za
kisiasa kuzuia safari hii zitakumbana na ukweli wa takwimu hizi. Ukweli
unaendelea kuangaza – na ukweli huo ni huu: Mama Samia ameahidi, na
ametekeleza.
0 Maoni