Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Wilaya ya Tanga Mjini wamemchagua mtia nia wa jimbo la Tanga Mjini ndugu. Ummy
Ali Mwalimu kwa kura 5,750 kati ya kura 10,293 zilizopigwa.
Akitangaza matokeo hayo ya kura za maoni jana Msimamizi wa uchaguzi
amesema kuwa Jimbo la Tanga Mjini linajumla ya wajumbe 12,620 na waliopiga kura
ni 10,293 ambapo kura zilizoharibika ni 117, kura halali zilizopigwa ni 10,176
sawa na Wastani wa asilimia 56.5.
Ummy Ali Mwalimu amepata kura 5,750 ambayo ni sawa na 56.5%, Omary Ayoub
akipata 4,146 sawa na 40%, Kassim Mbaraka 80 sawa na 1%, Rajabu Abasi 130 sawa
na 1% huku Arif Fazel akipata kura 70 sawa na 0%.
0 Maoni