Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Agosti 3, 2025 amefika kwa
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa
nafasi ya ubunge wa jimbo la Bukombe ikiwa ni sehemu ya utambulisho wa wagombea
wa udiwani na ubunge katika kata za Katente, Ng’anzo, Bulangwa, Namonge,
Busonzo, Runzewe Magharibi na Butinzya zilizopo jimbo la Bukombe.
Akizungumza mbele ya Wajumbe, Mbunge anayemaliza muda wake
Dkt. Doto Biteko amesema kuwa amerudi kwao akiamini kwamba wanachama wa Chama
Cha Mapinduzi na Wananchi wa Bukombe ndio wanatoa ridhaa kwa mgombea kupata
wadhifa huo.
“ Nawaambieni ukitaka kufanya kazi ya ubunge rudi kwa watu,
maana hii kazi ya ni ya Watu nenda kawaone wenye kazi yao, ndio maana kila
nikienda baada ya muda lazima nirudi, nilikuwa narudi kwa watu na mlivyokuwa
wema kila ninaporudi mnanipokea vizuri nafarijika”.
Aidha, Dkt. Doto Mashaka Biteko amesema kuwa miaka mitano
iliyopita ilikuwa miaka ya kazi iliyopambwa na ushirikiano wa kutosha miongoni
mwa viongozi na wanaCCM jambo lililokiwezesha Chama Cha Mapinduzi kupata
heshima kubwa na leo nimekuja kwenu kuwashukuru sana na kwa unyenyekevu mkubwa
ninawaomba kura zenu za ndiyo.
“Mimi sitaweka mawakala katika vituo vya kupigia kura kwa
sababu sina mashaka na nyinyi watu wema wa Bukombe bali mawakala wangu mtakuwa
ninyi wananchi wenyewe wa Bukombe”.
0 Maoni