Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Prof. Palamagamba
Kabudi ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo (WMA) katika Maonesho ya NaneNane
Dodoma na kuwapongeza watendaji wake kwa kazi nzuri wanayoifanya.
Mhe. Kabudi amesema WMA ni miongoni mwa Taasisi muhimu za Serikali zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja.
Ametoa rai kwa watendaji wa WMA kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili
kuwalinda walaji katika sekta zote nchini wakiwemo wakulima kupitia jukumu lao
kuu la uhakiki wa vipimo.


0 Maoni