Maafisa wa Kikosi kazi Taifa Dhidi Ujangili (NTAP) wametakiwa kutekeleza
mafunzo waliyoyapata kwa vitendo ili kukabiliana na ujangili na biashara haramu
ya nyara kwa ufanisi.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na
Utalii anayeshughulikia Maliasili, Kamishna wa Polisi Benedict Wakulyamba,
alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo washiriki kutoka
Kikosi kazi hicho, kulichofanyika Mtowaumbu Mkoani Arusha.
CP. Wakulyamba ameleza kuwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Mungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Maliasili na
Utalii, imeamua kuendesha mafunzo hayo kwa lengo la kuboresha na kuimarisha is
utendaji kazi kwa wataalam hao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya
kiteknolojia yanayotumiwa na wahalifu katika ujangili na biashara haramu ya
nyara.
“Mada zote mlizofundishwa katika mafunzo ya siku tatu, ni muhimu na
zitasaidia katika kupanua wigo wa kufanya kazi za intelijensia, ukamataji,
upelelezi na uendeshaji mashtaka kwenye mahakama zetu kwa weledi” Aliongeza CP.
Wakulyamba .
Kabla ya kufunga mafunzo hayo, CP. Wakulyamba alitoa mada inayohusu “
UCHUNGUZI WA ENEO LA TUKIO LA UHALIFU (CRIME SCENE INVESTIGATION)". Katika
Mada hiyo CP. Wakulyamba alifafanua masuala ya Kukagua, Kukusana na Kutunza
Vielelezo na Ushahidi unauohusishwa na Uhalifu kwenye eneo uhalifu
ulipotendeka.
Aidha, Katibu wa Kikosi Kazi Taifa Dhidi Ujangili (NTAP) ACP. Jumanne
Malangahe, ameushuruku Uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kuwezesha
kufanyika kwa mafunzo hayo, na kuahidi kuwa, watayatumia vyema katika ulinzi wa
rasilimali za wanyamapori na misitu nchini kwa manufaa ya kizazi cha sasa na
kijacho.
Na Sixmund Begashe – Mtwaumbu Arusha
0 Maoni