Wananchi wameendelea kumiminika katika banda la Mamlaka ya Eneo la
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) katika maonesho ya Nane Nane Jijini Dodoma kupata
elimu ya vivutio vya utalii, taratibu za kuingia hifadhini pamoja na huduma
mbalimbali zinazopatikana katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
Katika maonesho hayo wageni mbalimbali wanaotembelea banda la Wizara ya
Maliasili na Utalii katika maonesho ya Nanenane Dodoma wamepata fursa ya kushuhudia
vivutio vya utalii moja kwa moja kutokea Hifadhi ya Ngorongoro kupitia "TV
Screen" kubwa iliyofungwa katika banda la Wizara hiyo.
Maonesho ya Nane Nane yalianza Agosti 1,2025 na yanatarajiwa kufika
kilele chake Agosti 8,2025 yenye kauli mbiu " Chagua Viongozi Bora kwa
Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025".
0 Maoni