Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla, leo
Agosti 8, 2025 ametembelea Maonesho ya NaneNane kitaifa, uwanja wa Nzuguni
jijini Dodoma.
Akiwa katika Banda la WMA, Afisa Mtendaji Mkuu amewapongeza watumishi wa
Wakala kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma ambayo wamekuwa wakiifanya tangu
kuanza kwa Maonesho hayo.
Amewataka kuendelea kutoa elimu ya vipimo kwa jamii hata baada ya
Maonesho ili wananchi waelewe ni kwa namna gani Serikali kupitia WMA inawalinda
kwa kuhakikisha vipimo vinavyotumika katika sekta mbalimbali ni sahihi na
vinatumika kwa usahihi.
"Tuendelee kutumia majukwaa mbalimbali kutoa elimu ya vipimo kwa
wananchi ili waelewe haki yao ya kupata huduma kwa vipimo sahihi lakini pia na
wajibu wao wa kuhakikisha wanatumia vipimo sahihi katika sekta mbalimbali.
"
Kihulla ametembelea mabanda mengine mbalimbali likiwemo banda la Wizara
ya Viwanda na Biashara pamoja na Taasisi zake ili kujionea
huduma zinazotolewa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Bw. Alban Kihulla akimpatia
zawadi Afisa Mtendaji Mkuu Wa Usajili Wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey
Nyaisa leo Agosti 8, 2025 katika Maonesho ya NaneNane kitaifa, uwanja wa
Nzuguni jijini Dodoma.
0 Maoni