Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John
Nchimbi, akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari
leo Jumatatu Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu, Lumumba,
jijini Dar es Salaam, kuhusu harambee ya kuchangia kampeni za chama hicho
itakayozinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,
ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu
Hassan. Harambee hiyo inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya
maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na
kanga.
Dkt. Nchimbi amesema kwamba lengo la ni kuchangisha kiasi cha shilingi bilioni 100 na kuvitaka vyama vingine vya siasa pamoja na wanachama wa CCM na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kukichangia chama hicho
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Wahariri na Waandishi Waandamizi wa Vyombo vya Habari leo Jumatatu Agosti 11, 2025 katika Ofisi Ndogo ya CCM Makao Makuu, Lumumba, jijini Dar es Salaam, kuhusu harambee ya kuchangia kampeni za chama hicho itakayozinduliwa rasmi kesho katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Harambee hiyo inalenga kukusanya Shilingi Bilioni 100 kwa ajili ya maandalizi ya kampeni, ikiwemo gharama za magari, mabango, mafuta, fulana na kanga.
0 Maoni