Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atazindua rasmi Dira ya
Taifa ya Maendeleo 2050 leo katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini
Dodoma.
Dira hii ni mwongozo wa
muda mrefu wa maendeleo ya taifa, unaolenga kuiongoza Tanzania kuelekea kuwa
nchi yenye uchumi wa kati wa juu unaojali watu wake, mazingira na ustawi wa
kijamii na kiuchumi ifikapo mwaka 2050.
Dira ya Maendeleo 2050
imejikita katika nguzo kuu kadhaa, ikiwemo:
·
Ukuaji
wa uchumi jumuishi na shindani
·
Maendeleo
ya watu na rasilimali watu
·
Utawala
bora na utawala wa sheria
·
Uendelevu
wa mazingira na rasilimali asilia
·
Matumizi
ya teknolojia na ubunifu
0 Maoni