Kiongozi wa Mwenge wa
Uhuru Kitaifa Ndugu Ismail Ali Ussi leo
tarehe 16/7/2025 amezindua daraja la
watembea kwa miguu katika kitongoji cha Tripri, Kata ya Gehandu,Halmashauri ya
Mji wa Mbulu.
Ujenzi wa daraja hilo
limesaidia kuondoa utoro kwa wanafunzi wa eneo hilo ambapo awali walishindwa
kuhudhuria masomo hususan kipindi cha masika.
Aidha, daraja hilo
limekuwa mkombozi kwa wakazi takribani 4,000 kwa kuwarahisishia usafiri na
usafirishaji wa mazao.
0 Maoni