Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kimeeleza kuwa kimekamilisha maandalizi ya mkutano mkuu maalumu wa chama hicho
ngazi ya Taifa, unaotarajiwa kufanyika kesho, Julai 26, 2025, kwa njia ya
mtandao.
Akizungumza na waandishi
wa habari leo Julai 25, 2025 jijini Dodoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC) wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla amesema kuwa
maandalizi hayo yamefanyika kwa ufanisi katika ngazi zote za wilaya na mikoa
nchini.
“Mkutano huu maalumu
utafanyika kwa njia ya mtandao ili kurahisisha ushiriki wa wajumbe wote kutoka
maeneo mbalimbali ya nchi,” alisema Makalla.
Ameeleza kuwa mkutano huo
utaendeshwa kutokea jijini Dodoma na utatanguliwa na vikao vya Kamati Kuu
pamoja na Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
Akifafanua kuhusu ajenda
ya mkutano huo, Makalla amesema ajenda kuu itakuwa ni kujadili na kupitisha
marekebisho madogo ya Katiba ya CCM.
0 Maoni