WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu- Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete jana Julai
20, 2025 ameshiriki na kuhutubia Mkutano wa Vijana Wa Dunia uliofanyika katika
Mji wa Suzhou nchini China.
Kwenye Mkutano huo mkubwa
wa Dunia, Mhe. Kikwete ameeleza hatua mbalimbali ambazo zimefikiwa na Serikali
ya Awamu ya 6 ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha
vijana ikiwemo msisitizo mkubwa uliowekwa kisera, kisheria na mipango
mbalimbali ya kimaendeleo na ushirikishwaji wa vijana ikiwemo ile ya mgawanyo
wa asilimia 10 za mapato ya ndani ya Halmashauri na 4 kwa Vijana.
Mpango mwingine ni
asilimia 30 za fedha za manunuzi ya umma, mikopo ya uwezeshaji wa umma ikiwemo
ya NEEC, BEST, na hatua ya kushusha riba kwa wakopaji katika mabenki ya
biashara, uundaji wa Sera Mpya ya Vijana Nchini, Programu za maendeleo kama
BBT- Madini, Kilimo, Mifugo ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa kwa sasa kwa
Vijana wa Tanzania.
Mkutano huo uliomalizika
kwa mafanikio makubwa unakuwa ni mkutano wa 14 kukutanisha nchi wanachama na
unafungua fursa kwa nchi wanachama kukutana na kupeana uzoefu katika
kushughulikia changamoto mbalimbali zinazokabili vijana Duniani.

0 Maoni