TUME Huru ya Taifa ya
Uchaguzi (INEC) imewataka Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa,Wasimamizi wa
Uchaguzi,Wasimamizi wasaidizi ngazi ya Jimbo, Maofisa uchaguzi na maofisa
ununuzi kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo
mbalimbali yanayotolewa na tume hiyo.
Lengo la kusoma Katiba,sheria na maelekezo
mbalimbali yanayotolewa na Tume
hiyo ili yawaongoze katika kusimamia
vyema uchaguzi utakaokuwa huru na haki.
Mkurugenzi Msaidizi wa
Huduma za Sheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Cyprian Mbugano, alisema
hayo jana kwa niaba ya Mwenyekiti wa INEC, Jaji wa Rufaa, Jacobs
wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao wapatao 165
kutoka halamshauri 24 za mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro.
Katika mafunzo hayo mada
12 ziliwasilishwa kwa washiriki kujifunza , na
kauli mbiu ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 ni ‘ Kura yako, Haki yako,
Jitokeze kupiga kura”.
“ Kama ilivyoelezwa
wakati wa ufunguzi wa mafunzo haya , shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na
Katiba , sheria , kanuni , maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume hivyo
mkikutana na changamoto zozote msisite kufanya mawasilino na watendaji wa Tume,
” alisema Mbugano.
“ Jukumu lililo mbele
yenu ni kubwa na muhimu, linaahitaji umakini na kujitoa , hivyo ni matarajio ya
Tume kwamba , baada ya kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu yenu kwa
ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha Uchaguzi
Mkuu wa Oktoba Mwaka 2025 unaotarajiwa,” alisisitiza Mbugano.
Kwa upande wa ajira za
kupata watendaji wa vituo, alisema kuwa Tume inayoimani ya kwamba watateua na
kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hiyo muhimu , jambo ambalo limekuwa likisisitizwa tangu
mwanzo wa mafunzo hayo.
“ Watendaji hawa wa vituo
ndio watakaosimamia zoezi la kupinga kura na kuhesabu kura vituoni , kazi
ambayo inahitaji umahiri , umakini na weledi katika kuitekeleza,” alisisitiza
Mbugano.
Alisema ni imani ya Tume
kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yatafanyika kwa ufanisi na weledi katika
tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi na
yanalenga kuwajengea uwezo ili waweze kufahamu majukumu yao na kuyatekeleza ipasavyo wakati wa
uchaguzi.
Mbugano alitumia nafasi
hiyo kuwaasa wasimamizi hao kubandika matangazo mbalimbali ya kisheria kuhusiana
na uchaguzi pamoja na mabango mbalimbali yanayotakiwa kwa mujibu wa maelekezo.
Alisema ikumbukwe kuwa
,wapo wadau mbalimbali wa uchaguzi kama vile waangalizi wa uchaguzi kutoka
ndani na n je ya nchi ambao wanafuatilia uendeshwaji wa uchaguzi na kiwango cha
kuzingatiwaji wa sheria zinazohusiana na uchaguzi, hivyo wahakikishe
wanazigatia maelekezo yanayotolewa na
Tume kila wakati.
Akizungumza kwa niaba ya
washiriki wenzake, Mwenyekiti wa Mafunzo hayo, Dismass Pesambili aliishukuru
Serikali kupitia Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwawezesha mafunzo hayo ambayo
ni silaha na nyenzo muhimu ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa
Oktoba mwaka huu.
0 Maoni