Waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amezindua zoezi la Chanjo ya Mifugo katika
Kijiji cha Mokilal Tarafa ya Ngorongoro Mkoani Arusha ikiwa ni utekelezaji wa
mpango wa kitaifa wa miaka mitano wa kuchanja mifugo.
Dkt. Kijaji ameeleza
kuwa katika utekelezaji wa zoezi hilo ambalo ni mpango wa kitaifa wa Miaka
mitano kuanzia 2025-2030 ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Juni, 2025 Bariadi Mkoani Simiyu na
tayari kiasi cha shilingi bilioni 216 zimetengwa kufanya kazi hiyo na mwaka
huu zaidi ya Bilioni 62 imeshatolewa.
Amesema kuwa Serikali
imetoa punguzo la bei na kila Ng'ombe mfugaji atachangia shilingi 500 badala ya
shilingi 1000 na Mbuzi na Kondoo wafugaji watachangia shilingi 300 pekee
badala ya shilingi 500 ambapo mpango huu
unalenga kuwasaidia wafugaji.
Mkurugenzi wa huduma
za Mifugo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Benezeth Lutege ametaja Sababu za
kuchanja mifugo hiyo kuwa ni;
Kuongeza thamani
mifugo kwenye masoko ya nje, kujua idadi
ya mifugo na wamiliki wake ili kurahisisha upangaji wa maeneo ya malisho na
sababu nyingine kuwasaidia amana katika vyombo vya kifedha kupata mikopo kwa
kuwa taarifa za mifugo yao itakuwa
inatambulika mifumo ya kielektroniki (barcode)
kupitia alama ya hereni za utambuzi kwa kila mmiliki wa mifugo.
Kwa upande wake Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Kenan Kihongosi
ameeleza kuwa Wananchi wa Ngorongoro na Mkoa wa Arusha kwa ujumla wamekuwa na
muitikio mkubwa katika zoezi hilo na wataendelea kuhamasisha wafugaji wote
kuchanja mifugo yao ili kutimiza azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
kuboresha maisha ya Wananchi.
Mbunge wa Ngorongoro
Mhe. Emmanuel Shangai ameishukuru Serikali kwa kuwasikiliza Wafugaji na
kuwapatia chanjo ya mifugo yao na kuwaomba Wananchi wote kujitokeza kuchanja
mifugo hiyo ili kuondokana na maradhi mbalimbali, kuboresha afya na
thamani ya mifugo yao.
Na. Kassim Nyaki –
NCAA
0 Maoni