Hifadhi ya Mpanga Kipengere kuwania Tuzo za Kimataifa za mwaka 2026

 

Sekta ya utalii mkoani Njombe inapata msukumo mpya ambapo Hifadhi ya Pori la Akiba la Mpanga Kipengere imeingia kwenye mchuano wa kuwania tuzo za dunia (World Tourism Awards) katika vipengele vya sehemu bora ya fungate barani Afrika na sehemu bora ya utalii.

Hifadhi hii yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1,400 ina utajiri wa maporomoko ya maji yapatayo 50, bustani za asili za maua ya orchid, na maeneo ya kihistoria kama pango la Mtemi Mkwawa, jambo linalofanya eneo hili kuwa kivutio adhimu kwa watalii wa ndani na nje.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ufanisi wa miradi ya kimkakati iliyopo mkoani Njombe.

Alisema Serikali inaendelea kuimarisha miundombinu katika hifadhi hiyo pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Kituro inayojulikana kama 'Bustani ya Mungu', huku ujenzi wa hoteli na kambi za watalii ukihamasishwa ili kuongeza idadi ya vitanda na kujiandaa tayari kwa michuano ya AFCON 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.

Chapisha Maoni

0 Maoni