TARURA yashiriki Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji wilayani Ruangwa

 

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki kwenye maonesho ya madini na fursa za uwekezaji yanayofanyika katika uwanja wa madini wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Meneja wa TARURA mkoa wa Lindi, Mhandisi Fanuel Kalugendo ameeleza kuwa TARURA inaendelea kutekeleza ujenzi wa barabara zitakazofungua migodi inayopatikana katika wilaya hiyo ambapo barabara hizo zitajengwa kupitia mradi wa RISE unaogharamiwa na mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.

Barabara hizo zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni barabara ya Ruangwa - Mbwemkuru (Km 31) na barabara ya Nandagala - Mpiruka - Nachingwea (Km28) zilizopo wilayani Ruangwa.

Ameeleza kuwa wananchi mbalimbali wameendelea kufika katika banda la TARURA na kujionea kazi nzuri zinazofanywa na wakala katika kuboresha mtandao wa barabara mkoa wa Lindi.

Maonyesho hayo yaliyoanza tarehe 11 Juni, 2025 yamelenga kuonesha na kuwaelimisha wananchi fursa zilizopo wilaya ya Ruangwa hususani katika sekta ya madini.

Maonyesho hayo yanatarajiwa kufungwa leo siku ya Jumamosi tarehe 14 Juni, 2025 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.



Chapisha Maoni

0 Maoni