Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Bw. Hamad Abdallah, ametembelea na kukagua
maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi katika eneo la Medeli, Jijini Dodoma,
chini ya mradi wa Samia Housing Scheme.
Mradi huu
unatekelezwa kwa kasi na umedhamiria kutoa makazi bora na ya kisasa kwa
Watanzania, ikiwa ni sehemu ya mpango mkubwa wa ujenzi wa jumla ya nyumba 5,000
nchini. Tayari mpango huo umeanza kutekelezwa kwa mafanikio makubwa katika Jiji
la Dar es Salaam, eneo la Kawe, ambako nyumba 560 zimejengwa.
Katika hatua nyingine
ya utekelezaji, ujenzi wa nyumba za mradi huu umeanza pia katika eneo la
Kijichi, Dar es Salaam.
Samia Housing Scheme
ni mpango unaoenzi na kuendeleza maono ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuhakikisha Watanzania
wanapata makazi bora, salama na ya kisasa.
Kwa mara nyingine, Shirika la Nyumba la Taifa linaonesha dhamira ya dhati ya kutimiza wajibu wake wa kuwa msitari wa mbele katika sekta ya ujenzi wa nyumba za makazi, kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
#NHCTanzania
#SamiaHousingScheme #Dodoma #MakaziBora #KaziInaendelea #TanzaniaInawezekana
#UjenziWaMaendeleo
0 Maoni