WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi mahiri wa
Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa katika
sekta ya michezo kama sehemu ya utekelezaji wa Ibara ya 243 ya Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.
Pia, Waziri Mkuu
ametaja mafanikio yaliyopatika katika sekta ya michezo kuwa ni pamoja na
kuongezeka kwa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoka
shilingi bilioni 285 mwaka 2024/2025 hadi bilioni 519 katika mwaka wa fedha
2025/2026. “Ongezeko hili ni kubwa zaidi katika historia ya Wizara hii.”
“…Serikali imeendelea
na mkakati wake wa kuhakikisha inainua michezo hapa nchini, kila mmoja kwa
nafasi yake uwe mchezaji, wakala, mdhamini endelezeni taaluma hiyo. Leo hii
tuna kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru rais wetu kwa kufungua hiyo
milango na kuongeza bajeti na kuruhusu sekta binafsi kushiriki kwenye michezo.”
Ameyasema hayo jana
usiku (Jumapili, Juni Mosi, 2025) katika hafla ya usiku wa tuzo zilizoandaliwa
na Baraza la Michezo Tanzania kwa wanamichezo waliofanya vizuri kwenye
mashindano ya kimataifa iliyofanyika katika Ukumbi wa The Super Dome, Masaki,
jijini Dar es Salaam.
0 Maoni