Daktari wa
Kipalestina ambaye watoto wake tisa waliuawa katika shambulio la anga la Israel
huko Gaza tarehe 23 Mei, amefariki dunia kutokana na majeraha aliyopata katika
shambulio hilo hilo, maafisa wa afya wamesema.
Dkt. Hamdi al-Najjar
alikuwa amerudi baada ya kumpeleka mkewe, Dkt. Alaa al-Najjar, katika Hospitali
ya Nasser, ambako wote wawili walikuwa wakifanya kazi, wakati nyumba yao huko
Khan Younis ilipopigwa bomu. Watoto wao tisa waliuawa, huku mtoto wa kumi
akijeruhiwa vibaya.
Hamdi alilazwa
hospitalini na kutibiwa kutokana na majeraha ya ubongo na ya ndani, lakini
alifariki dunia siku ya Jumamosi. Alaa na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa
miaka 11, Adam, ambaye bado yuko hospitalini, ndio waliobaki hai katika familia
hiyo.
0 Maoni