Wizara ya Maliasili na Utalii imebainisha vipaumbele
10 ambavyo wizara na taasisi zake zitatekeleza kwa mwaka 2025/26.
Akiwasilisha mpango wa mapato na matumizi kwa Wizara na
taasisi zake kwa mwaka 2025/26, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi
Dkt.Pindi Chana amesema Wizara itatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maeneo
ya vipaumbele 10.
Amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kuendelea kutangaza
utalii ndani na nje ya nchi kupitia matangazo katika ligi kuu za michezo
mashuhuri duniani, mashindano ya kimataifa.
Pia kupitia mashirika ya ndege, misafara ya utangazaji
utalii, matamasha makubwa ya kimataifa na mitandao mbalimbali ya kimataifa na
vyombo vya habari.
Dkt. Chana amesema pia kuibua na kuendeleza mazao ya utalii
ya kimkakati ikiwemo maeneo ya malikale pamoja na utalii wa fukwe, mikutano na
matukio, meli, michezo, tiba na utamaduni.
Pia kuboresha miundombinu ya utalii na uhifadhi ikiwemo
barabara, viwanja vya ndege na huduma za utalii.
Dkt. Chana amesema pia kuimarisha matumizi ya teknolojia za
kisasa katika usimamizi wa uhifadhi na rasilimali, ufuatiliaji, utangazaji na
uendeshaji wa shughuli za utalii.
Pia kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa rasilimali za
wanyamapori, misitu, nyuki na malikale na kuongeza uzalishaji na thamani ya
mazao ya misitu na nyuki.
Dkt. Chana amesema pia kuendelea kuimarisha mifumo ya
upatikanaji wa takwimu mbalimbali, kufanya tafiti za kimkakati na kutoa huduma
za ushauri zinazohusu masuala ya uhifadhi endelevu wa wanyamapori, misitu na
nyuki, malikale na uendelezaji utalii.
Amesema vipaumbele vingine ni pamoja na uelimisha na kuhamasisha
jamii kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori,
malikale, misitu na ufugaji nyuki.
Pia kuimarisha usimamizi wa mifumo ya ukusanyaji wa mapato
yatokanayo na shughuli za utalii na uhifadhi.
Amesema pia kuandaa na kufanya Mapitio ya Sera, Sheria,
Kanuni na Miongozo mbalimbali ya kusimamia na kuendeleza Sekta ya Maliasili
na Utalii.
0 Maoni