Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba
amesema serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini ili ziweze
kutimiza majukumu ya msingi ya kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili
ya kuimarisha sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Elimu.
Mhe. Katimba amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma kwa
niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa
wakati akijibu swali la Mhe. Mwita Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini
aliyeitaka Ofisi ya Rais – TAMISEMI kutoa muongozo kwa Halmashauri kwa mwaka wa
fedha ujao ili kila Halmashauri iweke mpango wa kumaliza tatizo la meza, viti
na madawati.
Akijibu swali hilo Mhe. Katimba amesema “Nitumie nafasi hii
kuendelea kutoa msisitizo kwa wakurugenzi wetu wa Halmashauri zote 184 waweze
kutimiza wajibu wao wa msingi wa kutenga fedha kutoka kwenye mapato ya ndani na
kuweza kuziweka kwenye mipango na bajeti kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo.”
Katika hatua nyingine Mhe. Katimba amesema kwa mwaka wa fedha 2025/26 serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi bilioni 613 pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ili kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo upatikanaji wa madawati.
Na. OR- TAMISEMI
0 Maoni