Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 1.7 bilioni yamekamatwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari ljumaa usiku, Mei 23, 2025, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony
Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya
vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo
kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Said Mtanda,Vyombo vya usalama,uongozi wa
uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na
ya kizalendo ambayo wameifanya.
“Mtu
mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano
kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na
taratibu,” alisema Mhe. Mavunde.
Katika
tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban
USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa
yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa
lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.
Nitoe
rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya
biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo
ambayo hutaifishwa na serikali, alisema
Mavunde.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Saidi Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea
kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu
ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.
0 Maoni