Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko
Mei 15, 2025 ametembelea Bunge la Morocco ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya
kikazi nchini humo.
Akiwa Bungeni hapo, Dkt. Biteko amefanya mazungumzo na Spika
wa Bunge la nchi hiyo Mhe. Rachid Talbi El Alami na Naibu Spika Mhe. Lahcen
Haddad katika ofisi za Bunge hilo zilizoko jijini Rabat nchini Morocco.
Pamoja na mambo mengine, wamejadili kuhusu namna bora ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizo mbili hususan katika Sekta ya Nishati, Kilimo, Viwanda na Biashara
Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe Dkt. Doto Biteko akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Spika wa Morocco Mhe. Lahcen Haddad.






0 Maoni