Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) amepokea Maandamano ya wananchi pamoja na wapishi kutoka katika chuo Cha Utalii ikiwa ni ishara ya kuanza kwa jukwaa la pili la utalii wa Vyakula vya Asili, lililoandaliwa na shirika la Utalii duniani(UN Tourism) kwa Kanda ya Afrika. Mkutano huu utafanyika kuanzia tarehe 23 hadi 25 Aprili, 2025, jijini Arusha, katika Hoteli ya Gran Melia.
Naibu Waziri alipokea maandamano yao akiwa na Naibu Katibu Mkuu Utalii Ndugu Nkoba Mabula, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar na Mkurgenzi wa idara ya utalii wizara ya Maliasili na Utalii.





0 Maoni