Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto
Biteko leo Aprili 22, 2025 amewasili mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya kikazi
ya siku tano ambapo anatarajiwa kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na
wananchi kupitia mikutano ya hadhara.
Aprili 23 hadi 26, 2025 Dkt. Biteko atatembelea miradi ya
Maji, Elimu, Hospitali na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara
katika Wilaya za Arusha, Arumeru, Longido na Monduli.
Aidha, ziara hiyo ya kikazi ya siku tano ya Dkt. Biteko ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano.
Na. Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati




0 Maoni