Balozi Tembele azungumza na ujumbe ZEEA nchini Indonesia

 

Mapema leo, Mheshimiwa Macocha Moshe Tembele, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Indonesia amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi waandamizi kutoka Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) uliopo ziarani nchini Indonesia.   

Mheshimiwa Balozi ametoa wito kwa ujumbe huo kutumia ipasavyo fursa ya ziara yao hapa Indonesia ili waweze kupata uzoefu zaidi kuhusu namna Indonesia ilivyofanikiwa katika kuwawezesha wananchi wake kiuchumi na hatimaye kufanikisha malengo ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake Mheshimiwa Khamis Mwalim Suleiman, Katibu Mkuu, Afisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji alimshukuru Mheshimiwa Balozi kwa uratibu wa ziara pamoja na mapokezi mazuri waliyopata kutoka kwa maafisa wa Ubalozi pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali ya Indonesia zilizokusudiwa.

Ujumbe huo unahusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala  wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA) pamoja na menejimenti yake   unaendelea na ziara yake hapa Indonesia ambapo hadi sasa tayari umefanikiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi wa Wizara ya Uratibu wa Uwezeshaji Watu na Wizara ya Biashara ndogo ndogo na saizi ya Kati (SMEs) ya Indonesia.





Chapisha Maoni

0 Maoni