Waziri Masauni afanya ziara ya mafunzo Korea Kusini

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura. Waziri Masauni yupo nchini humo pamoja na viongozi wengine kwa ajili ya kujifunza masuala ya Biashara ya Kaboni. Machi 11, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (katikati), akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura (kulia). Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi. Waziri Masauni yupo nchini humo pamoja na viongozi wengine kwa ajili ya kujifunza masuala ya Biashara ya Kaboni. Machi 11, 2025.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini, Machi 11, 2025. Kulia ni Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura, wenginen katika picha ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Mkurugenzi wa Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) Prof. Eliakim Zahabu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni akizungumza na viongozi pamoja na wafanyakazi mara baada ya kuwasili Ubalozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini kwa ajili ya ziara ya kikazi, Machi 11, 2025. Kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania Nchini Korea Kusini Mhe. Balozi Togolani Mavura na kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Chapisha Maoni

0 Maoni