Kwa mara ya
kwanza katika historia ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ya mwaka
huu hapa nchini yanayofanyika katika
viwanja vya Saba Saba Mjini Njombe Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa
maonesho maalum ya mnyororo wa thamani wa sekta ya misitu pamoja na
Wanyamapori.
Kwa vipindi
tofauti wakikagua maandalizi ya siku ya Misitu Duniani kwenye maonesho Waziri
wa Maliasili na Utalii Mhe Pindi chana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi
wamefafanua kuwa Serikali imeamua kuwaleta Wanyamapori katika maonesho hayo ili
kutoa hamasa kwa wananchi kupenda utalii wa ndani.
"Tanzania
imebarikiwa kuwa na eneo kubwa la misitu takribani asilimia 50 ambalo ni makazi
ya Wanyamapori, hivyo tumeamua kuwaleta wanyama
wananchi waweze kupenda kutembelea hivyo kuliingizia taifa letu
fedha," amepongeza Mhe. Waziri
Naye Dkt.
Abbasi amewaarika wananchi kutembelea
maonesho ya Wanyamapori hao na
kwamba Serikali imetoa fursa ya wanyama
hao kuendelea kuwepo katika viwanja hivyo katika siku za mwisho wa juma hata
baada ya kilele hapo kesho ili wananchi wengi wapate fursa ya kuwaona.
Mgeni rasmi
hapo kesho ni Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Kauli mbiu ya
kitaifa ya mwaka huu ni ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa
raslimali kwa kizazi hiki na kijacho.
Na John
Mapepele - Njombe
0 Maoni