Rais Samia awanyooshea kidole wafanyakazi sekta ya ardhi

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema wafanyakazi waliopo katika sekta ya ardhi hawazungumzwi vizuri na wamekuwa wakihusishwa na rushwa.

Rais Dkt. Samia amesema hayo leo Machi 17, 2025 wakati akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023 kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete uliopo Jijini Dodoma.

Ameeleza kwamba miongoni mwa kero inayotajwa na wananchi katika wizara hiyo ni kuuza kiwanja kimoja mara mbili, hivyo teknolojia inayokuja ya utambuzi itasaidia kumaliza hilo na kuwataka kubadilika.

Pamoja na mambo mengine Rais Dkt. Samia amemuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratius Ndejembi, kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wa wizara hiyo wanaokwamisha utekelezaji wa majukumu na kusababisha malalamiko ya wananchi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Deogratius Ndejembi kwenye hafla ya uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 Toleo la 2023 na Mfumo wa e-Ardhi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma tarehe 17 Machi, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuashiria Uzinduzi  Rasmi wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya Mwaka 1995 toleo la Mwaka 2023 ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention center Dodoma leo Machi 17,2025.


Chapisha Maoni

0 Maoni