Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imekutana
leo Machi 18, 2025 Jijini Mbeya Kwa ajili ya kuanza kikao chake cha Kawaida cha
30 cha Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis
R. Semfuko.
Katika kikao
cha siku ya Kwanza (Leo) wajumbe wa kamati za Sera, Mipango na Fedha
inayoongozwa na Dr. Simon Mduma na kamati ya Ulinzi wa Rasilimali ya
Wanyamapori na Uendeshaji na Usimamizi wa Rasilimali watu inayoongozwa na Prof.
Jafari Kideghesho wamekutana na kujadili
masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo na ustawi wa Taasisi hiyo.
Aidha, kikao
hicho kinatarajiwa kufanyika Kwa siku nne ambapo Bodi itapata fursa ya
kutembelea Hifadhi ya Mpanga/Kipengere na kukagua miradi mbalimbali ya
maendeleo ikiwemo miundombinu ya utalii, miradi inayotekelezwa na
TAWA hifadhini humo.
Na. Beatus
Maganja - Mbeya
0 Maoni