Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kusini, Kamishna Msaidizi
Mwandamizi Godwell Meing’ataki amewataka watumishi wa Hifadhi ya Taifa Ruaha
kudumisha ushirikiano kwa uongozi mpya wa hifadhi hiyo.
Amesisitiza ushirikiano huo leo Februari 07, 2025 wakati wa
makabidhiano ya Ofisi kwa Mkuu mpya wa Hifadhi ya Taifa Ruaha ambaye ni Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi Abel Mtui, makabidhiano yaliyofanyika Makao Makuu ya
hifadhi hiyo yaliyopo Msembe ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.
Katika makabidhiano hayo Kamishna Meing’ataki alisema,
“Nawashukuru Maafisa na askari kwa ushirikiano mkubwa nilioupata kutoka kwenu
kwa kipindi chote cha uongozi wangu, tumeshirikiana katika mambo mengi mazuri
hivyo niwasihi endelezeni ushirikiano huo kwa uongozi huu mpya”.
Ikumbukwe kuwa Kamishna Meing’ataki aliyekuwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha kwa takribani miaka mitatu na hivi karibuni aliteuliwa kuwa Mkuu wa Kanda ya Kusini huku Kamishna Msaidizi Abel Mtui aliyepata uhamisho kutoka Hifadhi ya Taifa Katavi kwenda kuwa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Ruaha.



0 Maoni