Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Utalii, imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha wananchi
kuhusu wanyama wakali na waharibifu na kuwajengea vituo na kutoa vifaa vya
kukabiliana na changamoto hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ametoa shukrani
na pongezi hizo wakati kamati hiyo leo Februari 17, 2024 ilipokuwa ikitamatisha
ziara yake ya siku 3 katika Mkoa wa Tanga
kukagua mradi mbalimbali ambapo leo imekagua ujenzi wa kituo maalum cha kukabiliana na
tembo kilichokamilika kwa asilimia 100 katika kijiji cha Goha kata ya Mkumbara,
wilayani Korogwe.
"Tumeridhishwa
na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Rais wetu kupitia Wizara ya
Maliasili na Utalii katika kukabiliana changamoto hii katika kipindi kifupi,
kwa niaba ya kamati naomba nimshukuru na kumpongeza sana," amesisitiza
Mhe. Mnzava.
Kituo hicho
ambacho kimetumia milioni 48
kukamilika pia Serikali imetoa vifaa
yote muhimu ikiwa ni pamoja na samani,
ndege nyuki 1, gari 1 na askari sita ambao watakuwa kituoni hapo wakati wote.
Kituo hicho
ambacho kina vyumba vikubwa 3, Ofisi moja, jiko, bafu na choo kitasaidia
kukabiliana na changamoto hiyo katika vijiji zaidi ya kumi vinavyovunguka eneo
hilo.
Baadhi ya
vijiji vitakavyofaidika moja kwa moja na kituo hiki ni pamoja na Manga,
Mtitiro, Masira, Kwenangu, Mkomazi na Mikochen imeeleza taarifa ya Hifadhi ya
Ngorongoro, taasisi ambayo imepewa jukumu la kujenga na kusimamia.
Aidha, Mnzava
ameitaka Wizara kuhakikisha mara baada ya kukamilisha vituo hivyo kuleta vifaa
yote muhimu na watumishi wanaohitajika na wawepo muda wote.
Kamati hiyo iliambatana
na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu,
Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Katibu Mkuu, Kamishina wa Polisi, Benedict Wakulyamba
na watendaji kutoka wizarani na kwenye taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo.
Na. John
Mapepele - Tanga
0 Maoni