Jitihada za ufugaji
wa samaki kwa kutumia vizimba katika Ziwa Victoria zimeanza kuzaa matunda
kufuatia wavuvi wa Musoma Vijijini Mkoani Mara kuvuna tani tani 12 za samaki
wenye thamani ya fedha za Tanzania milioni 100.
Wavuvi hayo
wamemweleza Mbunge wao wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo wamepata
mavuno hayo ya idadi kubwa ya samaki kwenye kizimba kimoja chenye kipenyo cha
mita 10 (10m-diameter).
Ufugaji huo
wa samaki kwenye vizimba ni sehemu za jitihada za Prof. Muhongo za kuhakikisha
wakazi wa Musoma vijijini wanaendelea kunufaika na Ziwa Victoria ambalo ndilo
chanzo kikuu cha uchumi wa eneo hilo licha ya kuanza kuadimika kwa samaki.
Ziwa Victoria
lina umri wa takribani miaka 400,000 na ujazo wake wa kawaida ni kilomita za
ujazo 2,760 (2,760 cubic kilometres).
Mvua za mwaka
jana ziliongeza ujazo wa maji ndani ya bonde la Ziwa Victoria lenye ukubwa
kilomita za miraba 195,000 (195,000 square kilometres). Lilikuwa ongezeko la
kina cha takribani mita 1.7 (ca. 1.7 meters depth).
Ziwa Victoria ndani ya Jimbo la Musoma
Vijijini:
Kata 18 kati
ya Kata 21 za Jimbo letu zina ufukwe wa Ziwa Victoria. Kwa hiyo, asilimia 85.7
(85.7%) za Kata zetu zina fursa nzuri za kutumia raslimali za maji ya Ziwa
hili.
Samaki
wamepungua sana ndani ya Ziwa Victoria na mito inayolizunguka. Suluhisho la
tatizo hili ni kuanzisha na kuendeleza uvuvi wa ufugaji wa samaki ziwani humo
(aquaculture fish farming).
Upungufu wa
samaki haupo tu ndani ya Ziwa Victoria, bali ni tatizo kubwa ulimwenguni kote!
Bahari, maziwa na mito ya Duniani kote ina upungufu mkubwa wa samaki.
Kwa hiyo, kwa
sasa takribani nusu (ca. 50%) ya samaki Duniani kote wanapatikana kupitia
ufugaji wa samaki ndani ya bahari, maziwa, n.k. (aquaculture fish farming).
Uvuvi wa Vizimba Musoma Vijijini:
Malengo:
(i) Kata 18 kati ya 21 za Jimboni mwetu kuanzisha na kuendeleza Uvuvi wa Vizimba ndani ya Ziwa Victoria
(ii) Mitaji
ya Uvuvi wa Vizimba kupatikana kutoka:
(iia) Mitaji
ya watu binafsi: vizimba 10 vimeishaanza uzalishaji
(iib) Mitaji
kutoka mikopo nafuu ya Serikali Kuu: vizimba 8 tayari vimetayarishwa na kuwekwa
Ziwani. Uzalishaji utaanza ndani ya miezi 3 ijayo
(iic) Mitaji
kutoka mikopo mizuri ya Benki za Biashara (CRDB & NMB). Mikopo 10 ya
vizimba 50 itatolewa hivi karibuni.
Mafanikio ya awali ya Uvuvi wa
Vizimba:
Baadhi ya
wavuvi wa vizimba wa Musoma Vijijini wamemueleza Mbunge wao wa Jimbo kwamba,
kwenye kizimba kimoja chenye kipenyo cha mita 10 (10m-diameter) wamefanikiwa
kuvuna tani 12 za samaki wenye thamani ya Tsh milioni 100 (Tsh 100m).
0 Maoni